Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wazishauri nchi wanachama kuungana kutetea maslahi ya walemavu

Umoja wa Mataifa wazishauri nchi wanachama kuungana kutetea maslahi ya walemavu

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja huo kujiunga kwenye makubaliano ya shirika hilo ya kutetea haki za karibu watu milioni 650 walio na ulemavu wa aina moja au nyingine kote duniani.

Katibu anayehusika na masuala ya kiuchumi na kijamii kwenye Umoja wa Mataifa Sha Zukang ameuambia mkutano wa mataifa yanayounga mkono makubaliano hayo yaliyoanza kutekelezwa mwezi mei mwaka 2008 kuwa hadi sasa yamepata sahihi 146 ikiwa ni mara mbili zaidi na mwaka mmoja uliopita.

Sha Zukang ametoa wito kwa nchi wanachama zilizosalia kuwa wanachama wa makubaliano hayo akisema kuwa itakuwa rahisi kutekelezwa kwa makubaliano hayo ikiwa wanachama wote watashirikiana. Amesema kuwa watu walio na ulemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za umaskini na ukosefu wa ajira akiongeza kuwa ni jukumu la jamii ya kimataifa kulishughulikia suala hili. Makubalino hayo ni juhudi za kuhamikikisha kuwa walemavu wamepata haki zao zikiwemo za elimu, afya, ajira, mazingira wanamoishi na kutendewa haki kisheria kama watu walemavu.