Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu afungua chuo cha kwanza cha kupambana na ulaji rushwa

Katibu Mkuu afungua chuo cha kwanza cha kupambana na ulaji rushwa

Katibu Mkuu Ban Ki-moon alifungua rasmi hii leo chuo cha kimataifa cha kupambana na ulaji rushwa mjini Vienna.

Bw Ban anasema wakati mara nyingi ulaji rushwa umekua ukichukuiliwa kua ndiyio hali ya kawaida ya maisha hii leo mawazo yanabadilika kote duniani . Chuo hicho kinachogharimiwa kwa pamoja na serikali ya Austria, UNODC na afisi ya kupamban na rushwa Ulaya, kitakua na mipango kwa ajili ya maafisa wanaopambana na ulaji rushwa kutoka sekta za umma na binafsi kutoka hasa nchi zinazoendelea