Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa mabadiliko ya hali ya hewa anasema fedha ni muhimu kusaidia nchi zinazoendelea

Mkuu wa mabadiliko ya hali ya hewa anasema fedha ni muhimu kusaidia nchi zinazoendelea

Katibu mtendaji wa bodi ya mabadiliko ya hali ya Hewa ya Umoja wa Mataifa anasema ni uwongozi wa serikali pekee ndio utakaoweza kuepusha maafa makubwa ya baadae kutokana na mabadiliko hali ya hewa duniani, inayoashiriwa na mafuriko huko Pakistan, moto nchini Rashia na majanga mengine ya hali ya hewa huko Amerika, Asia na Afrika.

Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva Christiana Figueres, anasema fedha ndiyo msingi wa kusaidia mataifa yanayoendelea kufanya mabadiliko ya kutumia teknolojia ambazo ni nzuri kwa mazingira. Anasema mataifa tajiri yameweza kutambua mahala ya kupatikana mabilioni ya dola kwa ajili ya kugharimia mipango ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa mataifa maskini kabisa mwaka huu. Kiasin cha dola milioni 30 zimeahidiwa kutolewa ifikapo 2012. Bi Figueres anahisi hiyo inabidi kuchukuliwa kama idadi ya chini lakini alishuari kutozingatia haja ya kupatikana fedha zaidi:

(SAUTI YA FIGUERES)

Bi Figueres anasema hivi sasa kuna hali ya maelewano wanapojitayrisha kwa majadiliano ya Cancun mwishoni mwa mwaka huu.