Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupanda kwa bei ya ngano kwasababisha kupanda kwa bei ya vyakula duniani

Kupanda kwa bei ya ngano kwasababisha kupanda kwa bei ya vyakula duniani

Kuendelea kuongezeka kwa bei ya ngano kumesabababisha kupanda kwa bei ya vyakula kote duniani kwa asilimia tano mwezi uliopita na kuandikisha asilimia kubwa zaidi ya kupanda kwa bei ya vyakula kwa mwezi mmoja tangu mwezi Novemba mwaka uliopita.

Shirika la kilimo na mazao FAO linasema kuwa kupanda huku kwa bei ya ngano kwa asilimia tano pia kulichangia viwango vya juu zaidi vya bei tangu mwezi Septemba mwaka 2008 . Hali hii inatajwa kuchangiwa na kuwepo kwa hali ya kiangazi nchini urusi na marufuku iliyowekwa nchini humo ya kutouzwa nje kwa zao la ngano. Shirika la FAO pia linasema kuwa kuzalishwa kwa nafaka mwaka huu kutapungua kwa tani milioni 41 kutoka tani milioni 2279 hadi tani 2238 kote duniani. Pia kutokana na utabiri wa sasa ni kuwa huenda matumizi ya nafaka duniani yakazidi uzalishaji kati ya mwaka 2010 na 2011. Utabiri wa zao la ngano mwaka huu uliofanywa na shirika la FAO mnamo tarehe nne mwezi Agosti unaonyesha tani milioni 646 za ngano ikiwa ni chini ya asilimia tano ya kiwango cha mwaka uliopita.