Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na NGO's wanatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kuimarisha huduma za Afya Duniani

UM na NGO's wanatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kuimarisha huduma za Afya Duniani

Akiufunga mkutano wa 63 wa mashirika yasio ya kiserikali juu ya hali ya afya duniani huko Melbourne Australia Mary Norton, Mwenyekiti wa mkutano amesema,

Naye naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia mawasilianio Kiyo Akasaka, ametoa wito pia kwa wajumbe zaidi ya 1400 kuchukua jukumu la kuhamasisha utekelezaji wa MDG's wanaporudi nyumbani. Bw Akasaka anasema anamatumaini kwamba kila mjumbe atabeba mwenge wa mkutano kwa kutumia mafunzo walopata na kuwaelimisha wajumbe wao na jamii na kusaidia kuhamasisha juu ya hatari zilizopo kutofikia malengo ya milenia.

Mwenyekiti wa mkutano Bi Mary Norton amewahimiza wajumbe kuwasilisha mapendekezo ya tangazo lililoidhinishwa kwenye mkutano siku ya Jumatano kwa serikali za nchi zao ili ziweze kujumuisha katika mkutano ujao wa viongozi juu ya MDG's.

Zaidi ya hayo Bi Norton anasema wajumbe walikubali kuunga mkono mpango wa kuiruhusu Pakistan kutolipa kwa miaka miwili madeni yake kutokana na janga la asili linaloikumba nchi hiyo kwa wakati huu.