Umoja wa Mataifa unazindua mpango wa kupambana na biashara ya binadamu

31 Agosti 2010

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linakutana hii leo kuzindua rasmi Mpango wa Kimataifa wa Kuchukuliwa Hatua kupambana na biashara haramu ya binadamu. Akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu Ban Ki-moon anasema biashara haramu ya watu ni miongoni mwa ukiukaji mbaya kabisa wa haki za binadamu.

Bw Ban anasema hatua muhimu zimefanyika tangu Jumuia ya Kimataifa kuanza kupambana na janga hili miaka kumi iliyopita, lakini anasema kuna kazi zaidi zinahitajika.

"Njia pekee ya kukomesha biashara haramu ya binadamu ni kwa kufanya kazi pamoja, kwa ushirikiano kati ya mataifa na jumuia za kikanda, ushirikiano ndani ya Umoja wa Matiafa chini ya kundi la kuratibu ushirikiano wa idara mbali mbali, katika kupambana na biasharab haramu ya watu".

Katibu Mkuu anasema Mpango wa kuchukuliwa hatua utaasaidia kuzuia biashara ya watu, kuwahukumu wahalifu wa biashara hiyo na kuwalinda waathiriwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter