Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakuu wa UNICEF na WFP watatembelea maeneo ya mafuriko Pakistan

Wakuu wa UNICEF na WFP watatembelea maeneo ya mafuriko Pakistan

Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Chakula Duniani WFP, Bi. Josette Sheeran atafanya ziara ya siku mbili huko Pakistan, kutathmini jinsi kazi za shirika lake zinavyokidhi mahitaji ya mamilioni ya watu waloathirka na mafuriko, kuhakikisha uratibu mzuri na juhudi za serikali ya Pakistan na kuhimiza kuendelea kupatikana ungaji mkono wa kimataifa katika juhudi za msaada.

Wakati wa ziara yake itakayoanza kesho Jumanne, Bi Sheeran, atafuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya watoto ya Umoja wa Mataifa UNICEF Antony Lake, kuona jinsi idara hizo mbili zinavyofanyakazi pamoja kusaidia waathiriwa wa mafuriko.

Tangu kuanza mafuriko huko Pakistan mwishoni mwa Julai, WFP imeshawapatia watu milioni mbili na nusu resheni ya chakula ya mwezi mmoja. Wakati huo huo mataifa kadhaa ya Asia na ya Kiarabu pamoja na Australia na Hispania yamepeleka timu za watumishi wa afya ili kusaidia juhudi za huduma za afya katika maeneo yaliyoathitrika.

Asili mia 43 ya dola milioni 56.2 zilizoombwa kusaidia juhudi za afya imeshafika, na kufuatana na idara ya Huduma za Dharura ya Umoja wa Mataifa OCHA kumekuwepo na ongezeko la idadi ya watu wenye malaria katika majimbo ya Sindh na Baluchistan.