Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ingali ngumu kuweza kuwafikia wathiriwa wa mafuriko Pakistan :UM

Hali ingali ngumu kuweza kuwafikia wathiriwa wa mafuriko Pakistan :UM

Idara ya chakula duniani WFP inasema ingawa maji ya mafuriko huko Pakistan yameanza kupunguka katika maeneo mengi lakini uharibifu mkubwa wa miundo mbinu unezuia wafanyakazi wa huduma za dharura kufika katika maeneo yaliyo athirika. WFP hadi hivi sasa imeshatoa tani 24,000 za chakula cha dharura kwa watu milioni 2.

Kwa upande wake mratibu wa huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa anestahafu John Holmes, anasema hali inaendelea kua ngumu na ni changamoto kubwa kwa kila mtu kwa wakati huu.

"Kiwango cha mafuriko kinaendelea kuongezeka hasa huko kusini mwa jimbo la Sindh na kuelekea kusini mwa Pakistan, tukiwa na matumaini kwamba maji yatamwagika baharini hatimae kumalizika. Lakini hii inamaanisha kwamba watu wangali wanataabika huko.

Kwa wakati huo huo idara ya afya duniani WHO imesisitiza juu ya kuongezeka kulipuka kwa magonjwa katika maeneo yaliyoathirika. Hadi hivi sasa WHO imewatibu zaidi ya watu milioni 3.4.