Mkutano wa kimataifa wa vijana kuangazia masuala ya elimu, afya, ajira na uongozi.

24 Agosti 2010

Maelfu ya vijana, maafisa wa serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na maafisa kutoka Umoja wa Mataifa wanakutana katika mji wa Leon nchini Mexico juma hili kujadili masuala yanayohusu umaskini, afya, elimu, uhamiaji na siasa yaliyo muhimu kwa vijana kutoka nchi zaidi ya mia moja wanaohudhuria mkutano huo.

Suala kuu la mkutano huo wa kimataifa wa vijana unaondaliwa na serikali ya Mexico na Umoja wa Mataifa ni kuyapa kupaumbele mahitaji ya vijana. Hadi sasa kuna takriban watu bilioni 1.8 walio kati ya miaka 10 na 24 ambao ni robo ya watu wote duniani ambapo tisa kati ya vijana kumi wanaishi kwenye nchi zinazoendelea. Wataalamu wanasema kuwa kuwekeza katika sekta za elimu na afya kwa vijana ni muhimu zaidi kwa uchumi kwa kuwa wale wanaopata huduma hizo wanaweza kuchangia pakubwa kuinuka kwa jamii.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter