Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU yatoa wito wa msaada wa kifedha kusaidia maeneo yaliyioathirika na Mfurikom Pakistan

ITU yatoa wito wa msaada wa kifedha kusaidia maeneo yaliyioathirika na Mfurikom Pakistan

Katibu mkuu wa shirika la kimatia la mawasiliano ITU Hamadoun Toure ameto wito wa kimatiafa wa kuchangishwa fedha kusaidia wathiriwa wa mafuriko huko Pakistan.

Tume ya dharura ya mawasiliano ya ITU inafanyakazi pia na serikali ya Pakistan kukarabati miundo mbinu ya mawasiliano iliyoharibiwa kabisa katika sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Mafuriko yanayokumba Pakistan kwa wakati huu ni mabaya katika historia ya taifa hilo. Zaidi ya watu milioni 15 wamelazimika kuhama makazi yao na sehemu kubwa ya ardehi za kilimo zimeharibuiwa na maji.

Dk toure anasema dunia nzima imepigwa na butwaa kutokana na kuendelea kwa maafa hayo na kwamba ITU iko pamoja na watu wa Pakistan katika wakati huu mgumu wa mahitaji muhimu.

ITU kwa kawaida kutoa msaada wa dharura wa mawasiliano kufuatia maafa asili kama vile mtetemeko wa ardhi wa Haiti mwezi Januari pamoja na majanga mengine kote duniani.