Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amemteua mkuu mpya wa UN-Habitat

Ban amemteua mkuu mpya wa UN-Habitat

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameteua meya wa zamani wa Barcelona Joan Clos kuongoza idara ya Umoja wa Mataifa yenye jukumu la kuhamasisha mazingira muafaka na maisha bora ya kijami katika miji yote duniani.

Akiidhinishwa na Baraza Kuu, Clos kutoka Hispania, atakua mkurugenzi mpya wa Idara ya makazi ya Umoja wa mataifa UN-Habitat kwa kipindi cha miaka minne, na atachukua nafasi ya Bi Anna Tibaijuka aliyeongoza idara hiyo tangu 2001. Bw Clos mwenye umri wa miaka 61 alikua meya wa Barcelona kuanzia 1997 hadi 2006 na hivi karibuni alikua waziri wa viwanda, utali na biashara wa Hispania, na baadae balozi wa nchi yake huko Uturuki na Azerbaijan.

Lengo la UN-Habitat ni kuhakikisha kuna makazi ya kutosha kwa wote kwa kuhimiza maendeleo ya makazi bora katika miji mikubwa na midogo.