Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano na Henry Ndede kuhusu athari zinazoletwa na ukame na jangwa duniani

Mahojiano na Henry Ndede kuhusu athari zinazoletwa na ukame na jangwa duniani

Umoja wa Mataifa leo umezindua muongo wa vita dhidi ya ukame na jangwa duniani, vita ambavyo vina lengo la kuhamasisha na kuchagiza kuchukua hatua ili kuimarisha ulindaji wa maeneo makame ya dunia ambayo ni makazi ya theluthi moja ya watu wote duniani, na wanakabiliwa na tishio kubwa la kiuchumi na mazingira.

Katika ujumbe maalumu wa uzinduzi wa leo ambao kimataifa umefanyika Fortaleza Brazili katika jimbo la Ceara ambalo pia ni nusu jangwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ba Ki-moon amesema wakati tukianza muongo mzima wa vita dhidi ya ukame na jangwa tuongeze juhudi la kulinda ardhi ambayo tunaitegemea katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia na kutuhakikishia uhai wetu.

Flora Nducha wa Redio ya Umoja wa Mataifa amepata nafasi leo kumhoji Henry Ndede, mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Mpango wa Mazingira UNEP, Nairobi Kenya. Mratibu huo anafafanua kuhusu uzinduzi wa muongo wa vita dhidi ya ukama na jangwa na athari zake hususan barani Afrika.