Kifo cha Wangari Maathai ni pigo kubwa kwa Kenya:Odinga

Kifo cha Wangari Maathai ni pigo kubwa kwa Kenya:Odinga

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amesema kifo cha mwanamazingira wa Kimataifa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Profesa Wangari Maathai ni pigo kubwa kwa Kenya.

Akizungumza na idhaa hii leo amesema ingawa Bi Maathai mwenye umri wa miaka 71 alikuwa anasumbliwa na saratani lakini hakuna aliyetegemea angeaga dunia mapema kiasi hicho.

Waziri Odinga amesema Mchango wa Maathai nchini Kenya haupimiki na kwa heshima atapewa mazishi ya kitaifa. Odinga amezungumza kwa njia ya simu na Flora Nducha.

(MAHOJIANO NA WAZIRI RAILA ODINGA)