Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya vijana UN-HABITAT kufadhili miradi 51

Siku ya kimataifa ya vijana UN-HABITAT kufadhili miradi 51

Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT linatoa msaada kutoka mfufuko wake wa vijana mijini kwa miradi 51 iliyopendekezwa na vijana kote duniani.

Miradi iliyobahatika imepatikana kutoka maombi 1563 yaliyokusanywa toka nchi 85. India, Kenya na

Zimbabwe zilitoa idadi kubwa ya maombi yaliyofanikiwa chini ya mpango huo unaotoa misada ya dola milioni moja kkila mwaka. Miradi 51 iliyoshinda imetangazwa leo katika siku maalumu ya kimataifa ya vijana ambayo huadhimishwa kila mwaka Agost 12.

Miradi hiyo imeonyesha ubunifu mkubwa wa mawazo ya kuondoa umasikini, kuimarisha matarajio ya ajira kwa vijana na kuongeza uwezo wa vijana kushiriki katika michakato ya kidemokrasia. Mkurugenzi mkuu wa UN-HABITAT Bi Anna Tibaijuka akiwapongeza washindi amesema nayapongeza makundi yote ya vijana kwa miradi yao mizuri. Maombi yaliyoshinda yana mawazo mazuri ambayo kweli yatachangia katika ukuaji wa miji na nawatakia kila mafanikio katika miradi na maisha yenu ya baadaye.

Miongoni wa washindi wa msaada huo ni jumuiya ya Sierra Leone inayotoa mafunzo ya ufundi kwa vijana walemavu, Mtandao wa vijana wa Zimbabwe unaowawezesha vijana wa kwenye mabanda Zimbabwe kupata ardhi, Jumuiya ya vijana wa Palestina ilioanzsha baraza la kushawishi serikali za mitaa, jumuiya ya Haiti inayoanzisha kituo cha mafunzo ya mawasiliano ICT na kundi la vijana wa India linalotaka kuwawajibisha viongozi wa serikali za mitaa kupitia chombo cha habari cha wana nchi. Na fedha zinazotolewa kwa kila mradi ni kati ya dola 5000 na 25,000 na makundi yaliyoshinda na kupatiwa fedha hizo ni lazima yafuate vigezo vya Umoja wa Mastaifa na ynatakiwa kutoa ripoti ya matokeo na maendeleo ya mradi.