Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNAMID ajadili na viongozi wa Sudan hatma ya Kalma

Mkuu wa UNAMID ajadili na viongozi wa Sudan hatma ya Kalma

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani Darfur Sudan vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Ibrahim Gambari jana Jumatano alizuru eneo la Nyala na kutoa wito wa kudumisha amani.

Ziara hiyo ya Gambari Kusini mwa Darfur imefuatia machafuko ya karibuni katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kalma. Gambari katika ziara yake amekutana na maafisa wa serikali na kujadiliana nao njia muafaka ya kusonga mbele baada ya tafrani hiyo.

Gambari amefafanua pia taratibu zinazoongoza ushirikiano baiana ya UNAMID na serikali ya Sudan kifaifa na kimataifa na kusema moja ni hakuna mvutano kabisa na UNAMID haina mpango wa kuvutana na serikali, iwe ni ya Darfur Kusini au Khartoum. Ameongeza kuwa

(SAUTI YA IBRAHIMU GAMBARI)

Gambari pia amesema UNAMID inasimama kitedete na jukumu lake la kupokonya silaha katika kambi na amesema amewapa maelekezo wanajeshi wa UNAMID na polisi watajitetea watakaposhambuliwa na wahalifu.