Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LRA yaendelea na mauaji na utekaji DR Congo, Sudan na CAR

LRA yaendelea na mauaji na utekaji DR Congo, Sudan na CAR

Kundi wa waasi wa Uganda la Lord\'s Resistance Army LRA limeshutumiwa kuendelea na vitendo vya mauaji na utekaji hususan wa watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na INGO iitwayo imetosha yaani Enough, LRA imevamia eneo la Bas Uele nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kufanya mashambulio 51, yaliyosababisha vifo 105 kuanzia Aprili mwaka huu na kufanya idadi ya waliouawa na LRA DR Congo tangu 2008 kufikia 2500. Pia ripoti inasema watoto takribani 700 wametekwa kutumiwa na kundi hilo linaloongozwa na Joseph Kony katika mapigano kwenye nchi hizo tatu.

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Congo MUNUSCO una wanajeshi wake katika eneo la Dingila na wamesaidia licha ya uchache wao kupunguza mashambulizi ya LRA. Hata hivyo MUNUSCO inajiandaa kuondoa wanajeshi wake jambo ambalo linapingwa na wananchi wa Dingila wakihofia mashambulizi ya LRA.