Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zimepiga hatua katika mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa:Figueres

Serikali zimepiga hatua katika mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa:Figueres

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa klinachohusika na mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC Christina Figueres amesema serikali zinazokutana mjini Bonn Ujerumani zimepiga hatua katika kuamua muundo wa matokeo ya mkutano wa Novemba wa mabadiliko ya hali ya hewa utakaofanyika Cancun Mexico.

Amesema lakini sasa wanachohitaji ni kupunguza machaguo waliyonayo ili kuyafanyia kazi na kuyajadili. Katika mkutano wa Bonn ambao umemalizika leo serikali nyingi zimesema zinaamini masuala mengi yaliyofanyiwa maamuzi ambayo yatajumuiysha mipango ya Bali yanaweza kuwa na matokeo mazuri Cancun.

Bi Christiana amesema hii inamaanisha nchi zitakubali kuchukua hatua, kwa mfano kusimamia na kutoa fedha kwa ajili ya mambo ya hali ya hewa, kuinua kiwango cha teknolojia, kujenha ujuzi na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa hususan katika nchi masikini na zilizo katika hatari kubwa.