Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Duru ya tatu ya mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa imeanza Bonn

Duru ya tatu ya mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa imeanza Bonn

Duru ya tatu ya mazungumzo ya Umoja wa Mataifa ya mabadiliko ya hali ya hewa imeanza leo mjini Bonn Ujerumani.

Katibu mtendaji mpya wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCC, Christina Figueres amesema serikali zina wajibu mwaka huu kuchukua hatua katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Ameongeza kuwa ni kwa jinsi gani serikali zitafikia hatua hiyo ni juu yao, lakini ni kitu kinachowezekana kisiasa.

Ameendelea kusema mjini Cancun Mexico kazi ya serikali itakuwa ni kubadili linalowezekana kisiasa kuwa lisilogeuzwa kisiasa. Mazungumzo hayo ya wiki moja yana lengo la kutayarisha matokeo ya mkutano wa  kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa unakaofanyika mjini Cancun Mexico mwezi Novemba na Desemba.