Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amewataka wabunge kuendeleza ajenda ya kudhibiti silaha za nyuklia

Ban amewataka wabunge kuendeleza ajenda ya kudhibiti silaha za nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuna dalili za kupiga hatua kwenye mazungumzo ya uzalishaji wa nyuklia, na amewataka watunga sheria kuongeza shinikizo la kuisukuma mbele ajenda hiyo.

Ban akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa siku tatu wa maspika wa bunge mjini Geneva amesema hivi karibuni tumeona dalili za kupiga hatua kuhusu suala la uzalishaji wa nyuklia. Amesema tangu kundi hilo lililpokutana miaka mitano iliyopita dunia imekabiliwa na mambo mengi katika uchumi na chakula, pia migogoro inayoendelea kama vita DR Congo na Sudan, pia majanga asili mfano tetemeko la Haiti, na utengenezaji wa silaha za nyuklia, ugaidi na uhalifu wa kimataifa.

Ameongeza kuwa Marekani na Urusi wamehitimisha mkataba wa kupunguza silaha zao za nyuklia, hiyo ni hatua nzuri lakini juhudi zaidi zinahitajika.

(SAUTI YA BAN)