Ingawa hatua zimepigwa lakini bado vita dhidi ya ukimwi vinakabiliwa na changamoto:Ban

Ingawa hatua zimepigwa lakini bado vita dhidi ya ukimwi vinakabiliwa na changamoto:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kumepigwa hatua kubwa kimataifa kukabiliana na HIV na ukimwi.

Ban ameyasema hayo katika ujumbe maalumu kwa njia ya video kwenye mkutano wa kimataifa wa ukimwi ulioanza jana mjini Vienna Austria. Ban amesema maambukizi mapya yamepungua, wigo wa kuweza kupata dawa umeongezeka na vikwazo vya usafiri kwa waathirika vinaondolewa. Lakini ameonya kuwa pamoja na mafanikio bado kuna vikwazo vingi, kwani kuna baadhi ya serikali zinapunguza bajeti za kupambana na ukimwi.

(SAUTI YA BAN)

Amesema hatua hiyo inatia hofu na amewataka wote kuhakikisha kwamba mafanikio yaliyopatikana katika vita hivyo hayageuki. Naye Michel Sidibe mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS akizungumza kwenye mkutano huo amesema ana imani kuwa kwa pamoja dunia inaweza kutokomeza ugonjwa wa ukimwi

(SAUTI YA SIDIBE)