Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi waeleza mtazamo wa kuunganisha dunia kwa broadband:ITU

Viongozi waeleza mtazamo wa kuunganisha dunia kwa broadband:ITU

Wataalamu wa dunia kutoka viwandani, jumuiya za kijamii, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wabunifu, wamesisitiza jukumu la mtandao wa broadband katika maendeleo ya siku za usoni.

Wataalamu hao ambao wanaunda tume ya maendeleo ya tarakimu wametoa msisitizo huo mjini Geneva wanakokutana. ITU inasema makamishna hao wanakutana ili kufafanua mtazamo wa kuharakisha usambazaji wa mtandao wa broadband duniani kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma katika sekta za biashara na kijamii na pia kuchaapusha mchakato wa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Tume hiyo inaongozwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda,Carlos Slim Helu mwenyekiti wa kudumu wa Grupo Carso, Katibu Mkuu wa ITU Dr Hamadoun Toure na mkurugenzi wa UNESCO Irina Bokova. Tume hiyo itawasilisha matokeo yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon tarehe 19 Septemba mwka huu wakati wa mkutano wa malengo ya millennia kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.