Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa makabila ya asili wanaendelea kubaguliwa duniani:Pillay

Watu wa makabila ya asili wanaendelea kubaguliwa duniani:Pillay

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema watu wa makabila ya asili wanaendelea kubaguliwa katika maeneo yote duniani.

Amesema haki zao za kumiliki ardhi zinakiukwa na mara nyingi haki yao ya msingi ya kuishi. Bi Pillay ameyasema hayo katika ufunguzi wa kikao cha wataalmu kinachojadili haki za watu wa makabila ya asili.

Bi Pillay ameongeza kuwa mara nyingi wanabaguliwa katika ngazi za maamuzi na wanajikuta wakikabiliwa na matatizo makubwa.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)