Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia unaendelea kutengamaa lakini bado kuna hatari:IMF

Uchumi wa dunia unaendelea kutengamaa lakini bado kuna hatari:IMF

Ripoti ya shirika la fedha duniani IMF katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2010 inaashiria kiwango cha ukuaji wa uchumi kitaongezeka na kufikia asilimia nne na nusu.

Hata hivyo inasema kukuwa huko hakutodumu kwa muda mrefu sana kwani uchumi utaanza kushuka tena hadi asimilia nne na robo mwaka 2011 na kutakuwa na tofauti kubwa duniani kote. IMF imeonya kwamba licha ya kukua vizuri kwa uchumi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu , sintofahamu na hatari inayokabili ukanda wa euro inaweza kusambaa kwingineko na kusababisha hali ngumu kwa masuala ya fedha na mtazamo wa uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ripoti hii mjini Hong Kong, mwanauchumi mkuu wa IMF Olivier Blanchard amesema tunatabiri kuwa uchumi utaendelea kukua, lakini ni bayana kwamba hatari ya kuporomoka tena imeongezeka pia.