Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uingereza na jumuiya ya madola wametoa mchango mkubwa kwa UM:Ban

Uingereza na jumuiya ya madola wametoa mchango mkubwa kwa UM:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema katika utawala wa Malkia Elizabeth II Uingereza na jumuiya ya madola wametoa mchango mkubwa kwa Umoja wa Mataifa.

Ban ameyasema hayo jana alipomkaribisha Malkia Elizabeth II kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Ban amekumbusha kuwa zaidi ya nusu karne iliyopita Malkia aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba mustakhbali wa dunia utaundwa sio tuu na nguvu inayotuunganisha bali nguvu ya kujituma kwetu, kujituma kwa matumaini na mitazamo mizuri ya malengo ya Umoja wa Mataifa. Ban amemshukuru Malkia kwa kuhutubia tena Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu ameongeza kuwa leo hii makundi manne makubwa yanayochangia vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani yanatoka nchi za jumuiya ya madola. Na kote duniani wanafanya kazi na Umoja wa Mataifa kuleta maendeleo, kuchagiza haki za binadamu na kupigia upatu usalama wa kimataifa.