Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama linaweza na ni lazima liongeze juhudi kuwalinda raia:Ban

Baraza la usalama linaweza na ni lazima liongeze juhudi kuwalinda raia:Ban

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha hatua muhimu za kuwalinda raia katika maeneo ya migogoro.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameliambia baraza la usalama kwamba ametiwa moyo na hatua linazochukua ili kuhakikisha raia wanapewa kipaumbele katika masuala ya usalama. Ban ameyasema hayo wakati mjadala ukiendelea kuhusu kuwalinda raia katika migogoro ya kutumia silaha. Lakini amesisitiza pamoja na juhudi zilizofanyika baraza la usalama lazima lifanye juhudi zaidi za kuwalinda raia hao.

Kwanza amesema ni kutumia ipasavyo vikosi vya kulinda amani katika kuwalinda raia, na ameikaribisha juhudi za baraza hilo za kuongeza msisitizo katika kuwalinda raia hasa kwenye migogoro ya silaha.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Ban pia ameonya kwamba ili kutekeleza kwa mafanikio maeneo ambayo yana changamoto katika jukumu la kulinda amani baraza lazima litoe msaada wa kisiasa unaohitajika. Ameongeza kuwa wakati tunatafuta kuwalinda raia kutokana na athari za vita itakuwa busara pia kukabiliana na matarajio waliyonayo.