Skip to main content

El-nino imeanza kutoweka kwa mujibu wa shirika la hali ya hewa:WMO

El-nino imeanza kutoweka kwa mujibu wa shirika la hali ya hewa:WMO

Shirika la hali ya hewa duniani WMO linasema el nino imeanza kutoweka haraka mapema mwaka huu wa 2010 na kusababisha hali tulivu isiyo na nguvu ya la Nina kujitokeza katika mwambao wa Pacific.

WMO linasema inavyoonekana si rahisi kwa hali ya la Nina kuendelea zaidi katika miezi kadhaa ijayo kutokana  mabadiliko yaliyojitokeza.

Muda na ukubwa wa tukio la la nina kwa mwaka 2010 bado hauna uhakika, kwani hakuna dalili katika wakati huu kwamba kutakuwa na tukio la nguvu na kubwa hasa kwa kuangalia kiwango cha joto cha maji ya bahari.