Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India imeyataka mataifa kuzuia mashindano ya silaha katika anga za mbali

India imeyataka mataifa kuzuia mashindano ya silaha katika anga za mbali

India imeyata mataifa yote ambayo yana uwezo wa kutuma vifaa na silaha angani kuwa na jukumu la kuhakikisha malengo ya amani ya silaha hizo yanatekelezwa na kuzuaia mashindani ya silaha katika anga hizo za mbali.

Pia imesema kuepuka hatua zozote ambazo zinakwenda kinyume na malengo ya kutuma silaha hizo angani na kuzingatia mikataba iliyopo. India imeyasema hayo kwa niaba ya kundi la nchi 21 kwenye mkutano wa kimataifa wa upokonyaji silaha unaoendelea mjini Geneva.

Imeongeza kuwa kundi hilo imekuwa na hofu juu ya athari za kutengezeza na kutuma mfumo wa kujilinda wa makombora na watu kutafuta teknolojia ya hali ya juu ya kijeshi ili kutaka kuituma katika anga za mbali.Hamid Ali Rau ni balozi wa India.

(SAUTI YA HAMID ALI)