Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba mpya kusaidia athari za afya na mazingira wapitishwa

Mkataba mpya kusaidia athari za afya na mazingira wapitishwa

Mkataba mpya umepitishwa kuhakikisha kwamba masuala ya mazingira yanayohitaji kupewa kipaumbele yanajumuishwa katika mikakati ya mauamuzi ya serikali.

Mkataba huo unataka kuhusihwa kwa masuala ya mazingira katika sera za serikali ili kusaidia kulinda mazingira na kuchagiza maendeleo endelevu.

Mkataba huo ambao pia utakuwa unatathimini masuala yote ya mazingira uitwao UNECE Espoo Convention ulitiwa saini May 23 mwaka 2003 mjini Kiev Ukraine. Mataifa 35 yaliuridhia na utaanza rasmi kutekelezwa Julai 11 mwaka huu wa 2010.