Skip to main content

Malkia Elizabeth II kuhutubia Baraza Kuu la UM baada ya miaka 53

Malkia Elizabeth II kuhutubia Baraza Kuu la UM baada ya miaka 53

Malikia Elizabeth wa II wa Uingereza baadaye leo atahutubia Umoja wa Matifa ikiwa ni miaka 53 tangu aliposimama mbele kwa mara ya kwanza mbele ya hadhira ya wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1957.

Malikia Elizabeth mwenye umri wa miaka 84 hivi sasa alikuwa na umri wa miaka 31 tuu alipohutubia UM, na ilikuwa ni miaka mine tuu tangu alipotawazwa na kuvishwa taji la kuwa malkia.

Malkia Elizabeth ambaye anaambatana na mumewe Prince Philip safari hii katika hotuba yake kwenye Umoja wa Mataifa anatarajiwa kuuomba ulimwengu kudumisha amani na mshikamano.