Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC imehitimisha kikao cha mawaziri cha kila mwaka

ECOSOC imehitimisha kikao cha mawaziri cha kila mwaka

Baraza la uchumi na jamii ECOSOC limehitimisha mkutano wake wa tathmini wa mawaziri wa kila mwaka uliokuwa ukifanyika hapa New York.

Mkutano huo umeainisha mambo ya kufanya na hatua za kuchukua zenye lengo la kufikia ajenda ya kimataifa ya masuala ya wanawake wakati ambapo mjadala umewasikiliza wawakilishi kutoka nchi 50 wakielezea juhudi zao za kupigia upatu hali ya maisha , ajira na hatua za kijamii na kiuchumi walizopiga na haswa kwa wanawake na wasichana nyumbani na nje.

Mkutano wa mwaka huu pia umeonyesha hatua na mafanikio ya nchi 13 ambazo zimejitahidi katika sekta zote na kufikia malengo ya kimataifa katika masuala ya usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.