Skip to main content

Umoja wa Mataifa unaanzisha muundo mpya kwa ajili ya kuwawezesha wanawake

Umoja wa Mataifa unaanzisha muundo mpya kwa ajili ya kuwawezesha wanawake

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefiakia maafikiano yasiyo rasmi ya kuanzisha chombo maalumu kimoja cha kuchagiza usawa kwa wanawake. Katika hatua ya kihistoria leo baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepiga kura ya bila kupingwa kuanzisha chombo hicho ili kuvuta kasi ya mchakato wa kuyafanyia kazi mahitaji ya wanawake na wasichana kote duniani.

Kuanzishwa kwa kitengo hicho cha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake ambacho kitaitwa UN Women ni matokeo ya miaka mingi ya majadiliano baina ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na uelimishaji wa wanaharakati wa kupigania haki za wanawake.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amezungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya kihistoria. Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akikaribisha hatua hiyo amesema anawashukuru nchi wanachama kwa kuchukua hatua hii kubwa kwa ajili ya wanawake na wasichana kote duniani.