UM wamejadili jinsi utamaduni unavyoweza kusaidia na kuwa kikwazo kwa mwanamke

UM wamejadili jinsi utamaduni unavyoweza kusaidia na kuwa kikwazo kwa mwanamke

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA Thoraya Ahmet Obaid amesema utamaduni ni kuhusu kuhodhi mabadiliko na hakuna mabadiliko yatakayokuja kutoka nje.

Obaid alikuwa akizungumza katika mjadala wa kwanza kabisa wa moja kwa moja wa televisheni na kuongeza kuwa tamaduni zina nguvu kuliko utekelezaji wa sheria.

Ameelezea thamani ya jinsi utamaduni unavyompa hadhi mwanamke akihoji kwamba kama wanawake hawana haki za msingi kama kuzaa na afya ya uzazi watawezake kuwa na sauti kuhusu hatma yao?

(SAUTI YA THORAYA)

Washiriki wengine katika mjadala huo ni pamoja na mkurugenzi wa UNESCO Irina Bokova na walijadili uhusiano baina ya utamaduni na hadhi ya mwanamke, na kuangalia jinsi masuala ya uchumi, siasa na kijamii yanavyoathiri kuwawezesha wanawake.