Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO imezindua mtandao wa kimataifa wa miji kuwaenzi vikongwe

WHO imezindua mtandao wa kimataifa wa miji kuwaenzi vikongwe

Shirika la afya duniani WHO leo limezindua mtandao wa kimataifa wa miji kuthamini wazee kama sehemu ya kwenda sambamba na ongezeko la idadi ya vikongwe.

Kwa mujibu wa WHO kila kona ya dunia idadi kubwa ya watu wanazeeka, na mabadiliko makubwa yanatokea katika nchi zinazoendelea. Inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2050 asilimia 80 ya watu bilioni mbili wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 60 au zaidi wataishi katika nchi masikini au za kipato cha wastani.

WHO inasema lengo la mtandao uliozinduliwa leo ni kuisaidia miji kuweka mazingira ambayo yatawaruhusu vikongwe kuwajibika wakiwa na afya nzuri na kushiriki masuala mbalimbali katika jamii.