Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR amesisitiza kuboresha maisha ya wakimbizi Lebanon

Mkuu wa UNHCR amesisitiza kuboresha maisha ya wakimbizi Lebanon

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mastaifa wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Antonio Guterres amehitimisha ziara ya siku mbili nchi Lebanon kwa msisitizo wa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kuboresha maisha ya wakimbizi.

Amesema kikubwa na kuimarisha hali ya ulinzi kwa wakimbizi hao, baada ya kukutana na Rais Michele Suleiman, waziri mkuu Saad Hariri na maafisa wengine wa serikali. Bwana Guterres amesema anaelewa changamoto inayoikabili Lebanon ambayo inahifadhi wakimbizi wa Kipalestina laki tano. Akizungumzia wakimbizi 9200 ambao wametoka Iraq na Sudan na kusajiliwa na UNHCR Guterres ameelezea hofu yake juu ya sintofahamu ya hatima yao, na wasiwasi juu ya kukamatwa kwao, kuwekwa mahabusu na kurejeshwa nyumbani kwa nguvu.

Amesema mahabusu itumike tuu katika mazingira maalumu kama kuna hofu ya usalama. Pia amesisitiza wajibu wa UNHCR kutafuta suluhu kwa ajili ya wakimbizi hao ikiwa ni pamoja na kuwapatia makazi ya kudumu.