Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ameelezea hofu juu ya mipango ya kubomoa nyumba Mashariki mwa Jerusalem

Ban ameelezea hofu juu ya mipango ya kubomoa nyumba Mashariki mwa Jerusalem

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea hofu yake kufuatia taarifa kwamba manispaa ya Jerusalem ina mipango ya kubomoa nyumba zilizokuwepo na kujenga makazi zaidi ya walowezi katika eneo la Silwan mashariki mwa mji huo.

Ban amesema mipango hiyo ni kinyume na sheria za kimataifa na matakwa ya Wapalestina wanaoishi katika eneo hilo. Katibu Mkuu ameikumbusha serikali ya Israel kwamba ina wajibu wa kuhakikisha hatua za uchochezi hazichukuliwi, ambazo zinaweza kuongeza hali ya wasiwsi na mvutano katika mji huo.Ameongeza kuwa hatua hiyo haisaidii hasa katika wakati huu ambapo lengo ni kujenga imani ili kuunga mkono majadiliano ya kisiasa ya amani.

Duru zinasema manispaa hiyo imeidhiisha mipango ya kubomoa nyumba 22 za Wapalestina mjini Silwan kama sehemu ya kuliendeleza eneo hilo. Hivi karibuni maafisa wa Umoja wa Mataifa wameitaka Israel kusitisha ujenzo wote wa makazi ya walowezi na kutekeleza juhumu la mpango wa amani road map ambao umeidhinishwa kimataifa wa kuwa na suluhu ya mataifa mawili katika mgogoro huo wa mashariki ya kati.