Biashara zimetakiwa kusaidia na kupigia upatu haki za watoto

Biashara zimetakiwa kusaidia na kupigia upatu haki za watoto

Jumuiya ya wafanya biashara imetakiwa kushirikiana kujenga misingi ya kimataifa ambayo itaziweka haki za watoto katika jajenda ya juu ya ushirikiano wa jukumu la kimataifa.

Wito huo umetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa biashara na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, UN Global Compact, shirika la Save the children. Mkutano huo umeandaliwa na Umoja wa Mataifa. Mashirika hayo matatu yanawataka viongozi wa biashara kufanya kazi pamoja nao ili kuaweka sheria zitakazojulikana kama sheria za biashara kwa watoto ili ziweze kuepuka athari mbaya ambazo shughuli zao zinaweza kuzifanya kwa watoto, na badala yake zichangie kwa maisha mazuri ya baadaye kwa kila mmoja.

Mkutugenzi wa UNICEF Anthony Lake amesema kulinda haki za watoto ni jukumu la kimataifa ambalo linahitaji uwajibikaji kutoka kwetu sote katika kila sekta. Naye mkurugenzi wa UN Global Compact Georg Kell amekiri kwamba biashara ina fursa kuwa ya kuathiri maisha ya watoto.Taratibu zitakazowekwa zitazingatia mkataba wa haki za mtoto wa mwaka 1989 ambao unaainisha haki za msingi za binadamu kwa mtoto.