Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji katika malengo ya milenia ni uwekezaji katika uchumi imara

Uwekezaji katika malengo ya milenia ni uwekezaji katika uchumi imara

Viongozi wa masuala ya biashara wametakiwa kukubaliana katika mpango wa maendeleo ambapo makampuni yatafanya kazi kwa ushirika zaidi na Umoja wa Mataifa kufanikisha mipango na miradi mbalimbali.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa viongozi wa biashara (Global Compact Leaders Summit) hapa mjini New York. Amewataka viongozi kutambua kwamba kuwekeza katika malengo ya maendeleo ya milenia ni kuwekeza katika uchumi irama unaokuwa , akiongeza kuwa biashra itashamiri endapo tuu watu watashamiri.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Kwa siku mbili zijazo viongozi wa biashara watajadili ni wapi walipo na njia za kusonga mbele, kuyafanyia kazi yanayowezekana, kupeana changamoto za kujitahidi, kutaka ushirikiano wa kimataifa . Ban anasema watatoka na ajenda ambayo biashara itaunga mkono malengo ya maendeleo ya milenia.