Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaweza kabisa kuzuia adha ya Niger isiwe maafa makubwa: Holmes

Tunaweza kabisa kuzuia adha ya Niger isiwe maafa makubwa: Holmes

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa John Holmes amesema juhudi kubwa zinahitajika kuzuia adha ya Niger kugeuka na kuwa maafa makubwa.

Akizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa amesema hatua za haraka zinahitajika sasa hivi na katika muundo wa kuzuia nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi inayokabiliwa na ukame na ukosefu mkubwa wa chakula kuwa maafa ya kujutia kama ya mwaka 2005.

Ameongeza kuwa ni muhimu kujifunza kwa yaliyosibu 2005 na anaamini kuwa kuna uwezo wa kutosha kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na yasiyo ya kiserikali yaani NGO kuzuia maafa hayo yasitokee.

(SAUTI YA HOLMES)