Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna ongezeko la matumizi ya mihadarati katika nchi zinazoendelea: UNODC

Kuna ongezeko la matumizi ya mihadarati katika nchi zinazoendelea: UNODC

Ripoti ya kimataifa ya dawa za kulevya kwa mwaka huu 2010 inaonyesha matumizi ya dawa hizo yanahamia kwenye dawa mpya na masoko mapya.

Ripoti hiyo iliyotolewa leo na ofisi ya umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC inasema usambazaji wa kimataifa wa aina mbili za dawa zenye matatizo opiates na cocaine unaendelea kupungua.

Pia imebaini katika miaka miwili iliyopita ardhi iliyokuwa ikitumika kwa kilimo cha mimea ya kutengeneza dawa hizo duniani kote imepungua kwa asilimia 23. Lakini imeonya kuwa watumiaji wa dawa mpya aina ya amphetamine ni kati ya milioni 30 na 40 na idadi hiyo inazidi ile ya watuamiaji wa opiate na cocaine kwa pamoja.

Mkuu wa UNDOC Antonio Maria Costa amesema hatuwezi kutatua tatizo la dawa za kulevya kama tunabadili aina ya dawa kutoka heroine na cocaine na kuanza kutumia dawa zingine za kulevya ambazo pia zina madhara.