Skip to main content

Dunia inawataka wafanyakazi wa umma kuwa wabinifu zaidi:Ban

Dunia inawataka wafanyakazi wa umma kuwa wabinifu zaidi:Ban

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ya huduma kwa jamii na katika hafla maalumu mjini Barcelona Uhispania Umoja wa Mataifa umetoa tuzo kwa taasisi 23 za umma kutokana na mafanikio yake.

Baadhi ya taasisi hizo zimetumia tekinolojia kuongeza uwazi na uwajibikaji wa huduma wa serikali. Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuushinda umasikini, maradhi, ujinga , kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia na kufikia malengo ya milenia ifikapo 2015 tunahitaji kutoa kipaumbele katika huduma ya jamii.

Ameongeza kuwa ni lazima kuongeza ajira ya vijana wenye nia na ari ya kutumia ujuzi walionao wa kiteknolojia na kisayansi kwa malengo mazuri ya maendeleo.