Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon amesema hatua waliyopiga Sierra Leone ni mfano wa kuigwa

Ban Ki-moon amesema hatua waliyopiga Sierra Leone ni mfano wa kuigwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaja Sierra Leone kama moja ya mifano mikubwa ya kuigwa duniani kwa kupiga hatua baada ya machafuko na kudumisha amani.

Bwana Ban amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini humo ambako alikutana na Rais Bai Koroma na kuhudhuria mchezo wa kandanda kati ya vijana wenye ulemavu uliosababishwa na muongo mmoja wa vita nchini humo. Pia alizuru mahakama maalumu ya Sierra Leone iliyowekw kushughulikia uhalivu uliotekelezwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika 2002.

Ban alizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea shirika la utangazaji la nchi hiyo ambalo liliundwa kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari kuungana na kituo cha zamani cha utangazaji cha nchi hiyo na radio ya Umoja wa Mataifa inayojihusisha zaidi na mpango wa amani.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Bwana Ban amesema ujumbe wake ni kwamba pale ambapo viongozi na jamii wanaungana wanweza kupiga hatua katika masuala ya usalama na maendeleo. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kutoa msaada na kushirikiana na Sierra Leone katika juhudi za kujijenga upya.