Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo ya kiangazi inayoendeshwa na UNRWA imegunguliwa mjini Gaza

Michezo ya kiangazi inayoendeshwa na UNRWA imegunguliwa mjini Gaza

Michezo ya kiangazi kwa watoto wa Gaza chini ya mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa Palestina UNRWA imefunguliwa jana katika pwani ya Mediteranian.

Watoto laki mbili na nusu wanatarajiwa kushiriki katika michezo hiyo mbalimbali ikiwemo ya kuigiza, ngoma za asili, kuogelea, mpira wa wavu, mpira wa miguu na uchoraji.

Kufunguliwa kwa michezo hiyo mwaka huu kuna umuhimu mkubwa kwani Mai kituo hicho cha michezo kilishambuliwa na watu wenye itikadi kali, lakini UNRWA iliweza kukikarabati kwa wakati ili kufanya michezo hii. Mkurugenzi wa UNRWA John Ging anasema inatoa fursa nzuri kwa watoto na pia ulimwengu kujua kinachoendelea Gaza.

(SAUTI YA JOHN GING)