Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inahofia watoto wa Afghanistan wanotafuta hifadhi barani Ulaya

UNHCR inahofia watoto wa Afghanistan wanotafuta hifadhi barani Ulaya

Kamishna wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ameelezea wasiwasi wake juu ongezeko la watoto wa Afghanistan wanaofunga safari ngumu na ya hatari kwenda Ulaya kutafuta maisha bora.

UNHCR inasema zaidi ya watoto 5900 wa Kiafghanistan wengi wao wakiwa wavulana, walitafuta hifadhi Ulaya mwaka jana ikilinganishwa na 3,380 mwaka 2008. Utafiti wa UNHCR kuhusu watoto wanaosafiri bila mtu wa kuwasindikiza kuingia Ulaya unasema kwamba watoto mara nyingi wanasafiri bila wazazi wao na kujiweka katika hatari na kukiukwa haki zao.

Ripoti hiyo inasema mgogoro unaoendelea Afghanistan, umasikini uliotawala nchi hiyo,kutokuwepo na uongozi imara wa kisiasa , matumaini madogo ya elimu na kupoteza matumaini ya maisha bora ya baadaye vinachangia hali hiyo. Mkurugenzi wa UNHCR kwa Ulaya Judith Kumin anasema watoto wanakabilwa na hali ngumu wakiwa njiani lakini wanahisi wana wajibu mkubwa kwa familia zao , but feel na hivyo kuendelea na safari . Na matokeo yake wanakuwa wahang kila wakati.

Utafiti huo wa UNHCR umebaini kwamba vijana hao wa Kiafghanistan wanaowasili Ulaya sio wakati wote wanapata msaada unaohitajika na hivyo kuwalazimu wengi kuishia mikoni mwa wahalifu wnaowasafirisha kiharamu, na wengi huishia kwenye kambi kama za Calais Ufaransa na Patras Ugiriki.