Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na wadau wengine kulifanya kombe la dunia ushindi kwa watoto

UNICEF na wadau wengine kulifanya kombe la dunia ushindi kwa watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeanza kombe la dunia leo kwa kuwashirikisha wadau na kuandaa program maalumu katika mashindano hayo .

Program hiyo ni ya kuwapa watoto fursa ya kutambua uwezo wa michezo katika kuchagiza haki za watoto.

Katika mradi wa majaribio UNICEF inatoa nafasi kwa baadhi ya vijana kuangalia michuano ya kombe la dunia kupitia runinga kubwa zilizowekwa kwenye maeneo ya wazinchini Rwanda na Zambia .

Pia masuala ya elimu kuhusu haki za watoto na masuala ya ukiwmi yatazungumziwa.Joanne Dunn wa UNICEF anafafanua.