Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati jukumu la polisi wa UM likiongezeka, maafisa wanawake wanahitajika

Wakati jukumu la polisi wa UM likiongezeka, maafisa wanawake wanahitajika

Umoja wa Mataifa unaimarisha juhudi zake za kuongeza idadi ya maafisa wa polisi wanawake polisi katika mpango wa kulinda amani duniani kote.

Umoja wa Mtaifa unasema kwamba wanawake wanaweza kubeba jukumu muhimu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kukabiliana na ukatili wa kimapenzi na unyanyaswaji wa kijinsia. Idadi ya wanawake katika vikosi vya kulinda amani inaongezeka na Umoja wa Mataifa unalengo la kuongeza idadi yao zaidi ya mara mbili kwenye jeshi la polisi la Umoja wa Mataifa UNIPOL na kufikia asilimia 20 ifikapo 2014.

Mshauri wa polisi wa Umoja wa Mataifa Ann-Marie Orler leo amewaambia waandishi wa habari mjini New York kwamba kuendelea kukua na umuhimu wa jeshi letu la polisi kunabainisha jukumu muhimu la kuchagiza utawala wa sheria kwenye mazingira ya baada ya vita.

Mwezi wa nane mwaka jana Umoja wa Mataifa ulizindua juhudi za kimataifa kuongeza idadi ya maafisa wa polisi wanawake wanaoshiriki mpango wa kulinda amani hivi sasa kati ya walinda amani wa UNIPOL 17,407 wanaohudumu katika nchi 17 ni asilimia 8.5 pekee ambao ni wanawake.