Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea zimeshuhudia kuporomoka kwa biashara na nchi tajiri:ICT

Nchi zinazoendelea zimeshuhudia kuporomoka kwa biashara na nchi tajiri:ICT

Kituo cha kimataifa cha biashara ICT kimesema ingawa biashara kimataifa inaendelea kuimarika , nchi changa LDC\'S zimeshuhudia kuporomoka kwa biashara yake na nchi tajiri na zile zinazochipuka kiuchumi.

Katika ramani yake ya maendeleo ya biashara ya hivi karibuni shirika hilo linasema, kwa ujumla nchi zinazoendelea zimeona mabadiliko ya na kuimarika kwa biashara japo kidogo kwa mwaka 2004 na 2008 lakini 2009 mambo yakapinduka.

Ripoti hiyo inasema na mageuzi hayo yameonekana katika biashara na nchi tajiri kama Ulaya, Marekani na Japan na ile zinazochipukia kama Uchina na Brazili. Ripoti hiyo inasema biashara na nchi zinazochipukia kama Brazili na Uchina iliyumba kwa mwaka 2009 ikilinganishwa na biashara na nchi zilizoendelea kama Japan.