Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO inataka hatua za mapema zichukuliwe kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

FAO inataka hatua za mapema zichukuliwe kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema kilimo kinaweza kuwa sehemu ya suluhu ya mabadiliko ya hali ya hewa katika njia za kuheshimu na kusaidia mahitaji ya maendeleo na usalama wa chakula kwa nchi zinazoendelea.

Kauli hiyo ya FAO imetolewa kwa kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaoandaa mipango ya muda mrefu ya tazamo dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. FAO inasema ili kuhakikisha hilo linafanikiwa mjadiliano muhimu na yaliyopangwa vyema pamoja na maamuzi yanahitajika kufafanua njia zilizopo za kuzifanyia kazi na msaada unaotakiwa.

FAO imetoa wito wa kuchukuliwa hatua za mapema kuruhusu kilimo kusaidia na kuondoa gesi za viwandani hewani na kuwezesha kilimo katika mazingira magumu nay a hali mbya ya hewa ambayo yametabiriwa katika nchi nyingi masikini.