Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupunguza hatari ya majanga ni muhimu kwa mabadiliko ya hali ya hewa

Kupunguza hatari ya majanga ni muhimu kwa mabadiliko ya hali ya hewa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea umuhimu wa kupunguza hatari za majanga katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na kufikia malengo ya kuzitoa nchi zinazoendelea katika umasikini.

Katika ujumbe wake kwenye mkutano wa kimataifa wa hatari na majanga unaofanyika Davos Switzeland amesema tetemeko la ardhi la Haiti na majanga mengine ,mwaka huu ulianza vibaya na kutukumbusha hatari inayozikabili jamii na kujiandaa vyema.

Pia amegusia kwamba ataendesha mkutano kuhusu malengo ya milenia (MDG'S) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu ili kuchagiza kufikia malengo ya kupunguza jaa na umasikini, vifo vya watoto na kina mama wajawazito, na ukosefu wa elimu na huduma ya afya ifikapo mwaka 2015. huku serikali zikijiandaa kukutana Cancun Mexico mwezi Desemba kwa ajili ya mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa.