Matokeo rasmi ya uchaguzi wa udiwani Burundi yatoa ushindi kwa DNDD FDD

28 Mei 2010

Huko Burundi , Chama tawala cha CNDD FDD kimeibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika siku ya Jumatatu iliyopita.

Tume ya uchaguzi nchini humo imetangaza matokeo ya muda hii leo yanayokipa Chama cha CNDD FDD asilimia 64 ya kura, kikitangulia mbali sana Chama cha FNL kundi la mwisho la waasi zamani ,kilichopata asilimia 14 pekee.

Waangalizi wa kimataifa licha ya kupongeza uchaguzi huo , hata hivo vyama vya upinzani vinasema uligubikwa na wizi mkubwa wa kura na kuomba urejelewe. Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binaadamu Akich Okola amezitaka pande husika kuwa makini zaidi na kuweka mbele maslahi ya taifa. Kutoka Bujumbura ,Muandishi wetu Ramadhani Kibuga ametutumia taarifa hii.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter