Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa majadiliano kuchagiza amani

Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa majadiliano kuchagiza amani

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeangazia umuhimu wa mjadala kati ya mila kama njia mojawapo ya kuchangia amani duniani .

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa Ban Ki Moon ameonya kuwa duniani inazidi kuungana pamoja kupitia uhamiaji, biashara na teknolojia, lakini kwa upande mwingine pia dunia inazidi kutengana.

Ban katika hotuba yake kwa baraza la wanachama 15 ambapo mwenyekiti mwezi huu ni Waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri amesema, katiaka mazingira ambayo chuki imekithiri, wakati ambapo watu walio na misimamo mkali wanajaribu kupata watu ambao wataunga mkono mawazo yao wakitumia uchochezi dhidi ya watu wa kutoka eneo fulani na wakati ambapo wanasiasa wanajaribu kushinda katika uchaguzi wakitumia fitina, basi mjadala itakuwa ni muhimu.

Amesisitiza kuwa japo kuna utengamano baina ya watu ulimwenguni na watu wengi wakiwa kutoka asili mbali mbali, hali hii ni ya kusherehekewa, wakati huo huo inaweza kuwachanganya na kuwatia hofu watu wengine.